Tue, 22/03/2022 - 04:41

Kwa miaka kadhaa Kampuni ya Tanzania Portland Cement Ltd (Twiga Cement) imekuwa kinara katika usalama wa wafanyakazi wao sehemu zao za kazi. Hii inahakikisha ubora na kiwango cha juu katika uendeshaji wa shughuli yoyote ambayo inabidi ifanyike katika eneo la kazi la Twiga Cement.

Wanafunzi wa OSHA wamekuwa sehemu ya wageni katika machimbo ya Twiga na walijifunza mengi kuhusu usalama wa binadamu na mazingira (asili) kwa ujumla. Wanafunzi waliona mradi wa ukarabati uliofanywa na Twiga Cement kwa madhumuni ya kuleta uhai kwenye machimbo ya Twiga na kuhakikisha utatuzi wa changamoto unawezekana kwa lengo la kudumisha bioanuwai ya kipekee katika eneo la Machimbo la Wazo Hill ambayo imepotea kutokana na shuguli za uchimbaji wa malighafi za kutengenezea simenti.

Bw. Olais Raphael (Mshiriki wa QLA) aliwasilisha kuhusu Tuzo la Maisha ya Quarry (Quarry Life Award) na kuwakaribisha wafunzwa kuwa sehemu ya shindano lijalo kwa ajili ya kushinda tuzo na madhumuni ya kujifunza huku wakichangia kwa uhifadhi na maendeleo ya bioanuwai.

Twiga Cement inawakaribisha wadau mbali mbali kujifunza zaidi kuhusu Machimbo ya Wazo Hill na kuhakikisha uendelevu wa bioanuwai katika Maeneo ya Machimbo na Mashimo ya Changarawe.