Sat, 23/04/2022 - 18:05

Katika miaka ijayo Kituo kinatarajia kuhudumia walimu wapatao 500 katika Mkoa wa Dar es Salaam. Idadi hii ya walimu itawanufaisha vijana na watoto wapatao 25,000 kupitia klabu za mazingira za shule. Na hatimaye ikolojia ya jiji itatunzwa vyema na kulindwa kupitia watu binafsi ambao wamejengwa na kuhamasishwa kupitia maudhui ya dijitali yaliyohaririwa na wataalamu wenye uzoefu na kuwasaidia kuwa wahifadhi wa mazingira na asili.

Kituo hiki kitahudumia takriban wanafunzi 30+ kwa mwaka wa 2022 na walimu 6.

Karibu utembelee kituo hiki na ujipatie Cheti cha Mkufunzi wa Wanaasili kwa ajili ya kusaidia vijana na watoto shuleni kwako. Tembelea https://yes.mikoko.or.tz/qla.html